Sunday 15 June 2014

Published 04:33 by with 0 comment

EMMANUEL MBASHA NA FLORA MBASHA


Emmanuel Mbasha, mume wa mwimbaji wa injili Flora Mbasha hivi karibuni aliwashituwa watu mbalimbali baada ya kutuhumiwa kumbaka binti ambaye awali alitajwa kama mdogo wake Flora.

 
Akiongea na Global TV, Flora Mbasha amezungumzia tuhuma hizo na kuelezea kuwa kabla ya kufanya tukio hilo alikuwa hamuelewi kabisa mume wake ambaye Jumapili alimbadilikia kutoka na kile anachosema walikuwa wametofautiana na ndipo mumewe akafikia hatua ya kumkaba na kumtishia kumuua.

“Kabla sijatoka ndani alisema ‘we leo lazima nikufundisha adabu’, alinishika akaniniga yaani mpaka akaniachia maalama kwenye shingo yani hivi ninavyozungumza mpaka sasa hivi bado shingo yangu inaniuma hata kuongea siwezi.”

Mwimbaji huyo anadai kuwa mume wake hakuwa katika hali ya kawaida na baada yakumkataza asichukue gari Flora, mchungaji Gwajima alimpigia simu na kisha kumtumia gari afike kanisani na watoto aliokuwa amemwambia awapeleke.
  

Hata hivyo hatua hiyo ilimchafua zaidi Emmanuel ambaye alipiga simu na kutukana matusi muda mrefu tena matusi ya nguoni.
 
Ameeleza kuwa siku hiyo hakurudi nyumbani na siku iliyofuata ndipo binti huyo amedai sio mdogo wake bali walikuwa wanaishi nae alimpigia simu ndugu yake Flora na kumpa mkasa wa kubakwa na kusababishiwa maumivu na bwana Mbasha.

“Huo usiku sikurudi nyumbani na asubuhi Jumatatu yule binti akapiga simu, hakunipigia mimi akampigia mdogo wangu mwingine akamwambia mimi naondoka mimi shemeji ameninyanyasa amenidhalilisha kanifanyia kitendo kibaya sana, sasa akamuuliza amekufanyia nini? 


"Akawa hawezi kuongea kwenye simu akamshauri tu kwamba usiondoke subiri dada yako atakapokuja kwanza anarudi muda si mrefu…Kwa sababu yule binti tulikuwa tunakaa nae nyumbani namtunza mimi. 


"Kwa hiyo nilikuwa naishi nae hapo ndani kwa hiyo alikuwa kama ni mtoto wa kwangu mimi tulikuwa tunamlea pamoja na mme wangu.”

 
Hadi sasa bado mume wa Flora hajapatikana na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo za ubakaji.


Tazama  video  ya  mahojiano  hayo  hapo  chini.
      edit

0 comments:

Post a Comment