Hausigeli
aitwaye Melina Mathayo mwenye umri kati ya miaka 15, ameumizwa vibaya sehemu za
kichwani na kulazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada
ya kupigwa na bosi wake aitwaye Yasintha Rwechungura mkazi wa Boko.
Akiongea na
mwanahabari wetu akiwa katika hospitali hiyo, Melina amesema amekuwa akipigwa
na bosi wake huyo mara kwa mara kwa kutumia waya, brenda na vifaa vingine japo
alikuwa akiogopa kusema.
Vitendo hivi vya
ukatili vinaonekana kushamiri kwa sasa ikiwa ni siku chache baada ya hausigeli
aitwaye Yusta kuripotiwa kung'atwa na bosi wake aitwaye Amina Maige
aliyepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
Binti huyo
aliyeletwa Mwananyamala jana alfajiri akiwa na hali mbaya amefanya kazi kwa
miaka miwili nyumbani kwa mama huyo mwenyeji wa mkoani Kagera.
Melina alikuwa
akiongea na mwanahabari wetu akiwa na mpira wa kuongezewa damu mwilini na
amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment