Msomi Joshua Sanga hatimaye ameaga ukapera siku ya Ijumaa Tarehe 13/06/2014, Mungu awatangulie katika Maisha yenu mapya ya ndoa. Amina
Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts
Sunday, 15 June 2014
Msomi Joshua Sanga hatimaye ameaga ukapera siku ya Ijumaa Tarehe 13/06/2014, Mungu awatangulie katika Maisha yenu mapya ya ndoa. Amina
Akiongea na Global TV, Flora Mbasha
amezungumzia tuhuma hizo na kuelezea kuwa kabla ya kufanya tukio hilo alikuwa
hamuelewi kabisa mume wake ambaye Jumapili alimbadilikia kutoka na kile
anachosema walikuwa wametofautiana na ndipo mumewe akafikia hatua ya kumkaba na
kumtishia kumuua.
“Kabla sijatoka ndani alisema ‘we leo
lazima nikufundisha adabu’, alinishika akaniniga yaani mpaka akaniachia maalama
kwenye shingo yani hivi ninavyozungumza mpaka sasa hivi bado shingo yangu
inaniuma hata kuongea siwezi.”
Mwimbaji huyo anadai kuwa mume wake
hakuwa katika hali ya kawaida na baada yakumkataza asichukue gari Flora,
mchungaji Gwajima alimpigia simu na kisha kumtumia gari afike kanisani na
watoto aliokuwa amemwambia awapeleke.
Hata hivyo hatua hiyo ilimchafua zaidi Emmanuel ambaye alipiga simu na kutukana matusi muda mrefu tena matusi ya nguoni.
Ameeleza kuwa siku hiyo hakurudi
nyumbani na siku iliyofuata ndipo binti huyo amedai sio mdogo wake bali
walikuwa wanaishi nae alimpigia simu ndugu yake Flora na kumpa mkasa wa kubakwa
na kusababishiwa maumivu na bwana Mbasha.
“Huo usiku sikurudi nyumbani na asubuhi
Jumatatu yule binti akapiga simu, hakunipigia mimi akampigia mdogo wangu
mwingine akamwambia mimi naondoka mimi shemeji ameninyanyasa amenidhalilisha
kanifanyia kitendo kibaya sana, sasa akamuuliza amekufanyia nini?
"Akawa hawezi kuongea kwenye simu akamshauri tu kwamba usiondoke subiri dada yako atakapokuja kwanza anarudi muda si mrefu…Kwa sababu yule binti tulikuwa tunakaa nae nyumbani namtunza mimi.
"Kwa hiyo nilikuwa naishi nae hapo ndani kwa hiyo alikuwa kama ni mtoto wa kwangu mimi tulikuwa tunamlea pamoja na mme wangu.”
Hadi sasa bado mume wa Flora
hajapatikana na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo za ubakaji.
Tazama video ya mahojiano hayo hapo chini.
Hausigeli
aitwaye Melina Mathayo mwenye umri kati ya miaka 15, ameumizwa vibaya sehemu za
kichwani na kulazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada
ya kupigwa na bosi wake aitwaye Yasintha Rwechungura mkazi wa Boko.
Akiongea na
mwanahabari wetu akiwa katika hospitali hiyo, Melina amesema amekuwa akipigwa
na bosi wake huyo mara kwa mara kwa kutumia waya, brenda na vifaa vingine japo
alikuwa akiogopa kusema.
Vitendo hivi vya
ukatili vinaonekana kushamiri kwa sasa ikiwa ni siku chache baada ya hausigeli
aitwaye Yusta kuripotiwa kung'atwa na bosi wake aitwaye Amina Maige
aliyepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
Binti huyo
aliyeletwa Mwananyamala jana alfajiri akiwa na hali mbaya amefanya kazi kwa
miaka miwili nyumbani kwa mama huyo mwenyeji wa mkoani Kagera.
Melina alikuwa
akiongea na mwanahabari wetu akiwa na mpira wa kuongezewa damu mwilini na
amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Maria Said mama mkubwa wa Nasra, (katikati) ni baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na (kulia) ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya box kwa miaka 4 baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa Malaria.
MUME na mke wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4 ndani ya Box .
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika Mei 20 mwaka huu majira ya saa 4.45 Asubuhi katika eneo la mtaa Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.
Alisema majirani walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria Said na kutaka kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika nyumba hiyo na kukuta mtoto huyo akiwa katika box.
Alimtaja mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi minne na nusu ambapo polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii ili kuendela nayo.
Afisa Ustawi wa jamii katika ofisi ya mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu alisema mtoto huyo alipelekwa hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa sababu alionekana kuwa na afya dhoofu.
Muuguzi katika Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.
Alisema alilazwa na kwamba kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii huku wakiwachukulia hatua za kisheria walezi wa mtoto huyo Mariam Said na Mume wake Mtonga Omari.
Baba mzazi wa mtoto huyo alisema yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.
Alisema kila mara alikuwa akifika kumwona mtoto mama huyo alimwambia mtoto kalala na hivyo kushindwa kumwona na kujua hali halisi hadi siku ya tukio na kwamba alikuwa akimpatia matumizi ya mtoto huyo.
Ofisa mtendaji wa kata hiyo Dia Zongo alisema akiwa katika kazi za kawaida katika Mtaa wa Azimio, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke huyo, alimficha mtoto Nasra ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
Zongo alisema baada ya kupata taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kuanza kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika na kushindwa kueleza ukweli juu ya kuwepo kwa mtoto huyo.
Zongo alisema wakati mtuhumiwa akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasrah akiwa ndani ya boksi nyuma ya mlango .
Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama yake huyo mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe, walianza kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha (mtendaji) kutoa taarifa polisi.
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
Mtuhumiwa huyo alisema kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka jana na kwamba alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa limewekwa nyuma ya mlango wa chumba cha mwanamke huyo.
Hores Isaack Msaky Dk Mshauri wa watoto katika hospitali ya mkoa wa Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa matibabu ya awali .
‘’ Tulimfanyia vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na Nimoni pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema
Alisema bado wanaendela na vipimo vingine vya XRay kubaini mtoto huyo alipata ulemavu kwa kupigwa au alizaliwa hivyo.
Alisema mtoto huyo anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili wake pia ni mteke kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela kumfanyia uchunguzi wa kina zaidi.
Baadi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki dunia miaka mine iliopita na kwamba Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto huyo.
Hata hivyo majirani hao walidai wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina kutokana na kwamba mama huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti na mtoto huyo.
Source Tanzania Today...
Subscribe to:
Posts (Atom)






